Serikali kuwa huru kuchagua vyombo vya kupeleka matangazo

0
333

Bunge la Tanzania leo linajadili na kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ambapo miongoni mwa marekebisho yanayotarajiwa kufanyika ni kumwondolea Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Habari jukumu la uratibu wa matangazo ya Serikali.

Pia, muswada unalenga kuiwezesha Serikali kuwa na uhuru wa kuchagua chombo cha habari itakachotumia kwa ajili ya matangaza kwa kuzingatia ushindani katika soko.

Marekebisho mengine ni kuongeza uhuru wa maoni katika kifungu cha 38, na pia kuwe na adhabu tahafifu kwa makosa yatokanayo na ukiukwaji wa sheria hiyo kuwafanya wanahabari kujirudi na kufurahia kazi zao.

Aidha, marekebisho pia yanakusudia kuondoa adhabu kwa wamiliki wa mitambo ya uchapishaji, ambao katika hali ya kawaida, hawana uwezo wa kudhibiti maudhui yanayochapishwa katika mitambo hiyo.