Serikali kutumia hekima zoezi la kufungia laini

0
1251

Saa chache kabla ya kufungiwa kwa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama ya vidole, serikali imesema itatumia hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini zao kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa au namba licha ya kuanza mchakato wa kupata kitambulisho hicho.

Hayo yameelezwa jana, Januari 19 na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa CCM mkoani Kigoma.

Amebainisha kuwa wananchi walioomba vitambulisho/namba lakini bado hawajapata, taarifa zao zipo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), hivyo wao kushindwa kusajili laini ni jambo lililo nje ya uwezo wao.

“Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa.”

Nditiye ameongeza kuwa watakaofungiwa laini zao ni wale wenye vitambulisho lakini hawajazisajili.