Serikali kutoa Elimu kwa wenye mahitaji maalum

0
274

Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa watoto wenye mahitaji maalum wanapata huduma zote stahiki ikiwemo elimu kama ilivyo kwa wanafunzi wengine.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo leo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye shule ya sekondari Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam.

Prof. Mkenda ametoa mwito kwa watanzania wote hususani wazazi kutowawaficha ndani watoto wenye mahitaji maalumu badala yake wawapeleke shule ili waweze kupata elimu.

Amesisitiza kuwa serikali imekamilisha ujenzi wa shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara pamoja na Arusha na shule nyingine ambayo ujenzi wake unaendelea mkoani Geita.