Serikali kupunguza gharama za upasuaji

0
123

Serikali ipo katika mapitio ya bei za upasuaji katika hospitali za serikali, ili kutoa nafuu kwa wananchi ambao wanalazimika kupatiwa huduma hiyo.

Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange ameliambi Bunge jijini Dodoma kuwa, serikali imepokea maoni ya wananchi kuhusiana na bei ya kufanya upasuaji na wanaendelea kuzifanyia mapitio ili ziwe na nafuu kwa wagonjwa.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Temeke Doroth Kilave, Dkt. Dugange amesema, ni kweli bei hizo zimekuwa kubwa na kwa sasa serikali inazifanyia mapitio ili kutoa unafuu kwa wananchi.

Kuhusiana na upungufu wa dawa kwenye baadhi ya hospitali za serikali, Naibu waziri Dugange amesema, serikali imeendelea kusimamia upelekaji wa dawa japo kuna changamoto kadhaa ambazo bado wanaendelea kuzifanyia kazi.