Serikali kupitia upya ushuru wa mchele

0
150

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji
amewaahidi Wafanyabiashara wa soko la mchele la Magugu mkoani Manyara kufanyia kazi kero ya utozaji wa ushuru wa shilingi 1, 500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50.

Waziri Kijaji ametoa ahadi hiyo alipotembelea soko la mchele la Magugu kwa lengo la kukutana na Wafanyabiashara na kujionea hali ya biashara katika soko hilo.

Wakizungumza na Waziri Kijaji baadhi ya Wafanyabiashara wa soko hilo la mchele la Magugu wameipongeza Serikali kwa kusaidia kuboresha mazingira ya wafabyabiashara wadogo na wameiomba Serikali iwapunguzie tozo ya ushuru wa shilingi 1, 500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50 kwa kuwa inaongeza gharama katika biashara.