Serikali kukamilisha vigezo vya kuifanya Chato kuwa mkoa

0
226

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kukamilisha vigezo muhimu vinavyoruhusu kuifanya wilaya ya Chato kuwa mkoa.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita, wakati wa sherehe za kilele cha mbio maalum za Mwenge wa Uhuru, kumbukizi ya miaka 22 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kilele cha wiki ya Vijana kitaifa.
 
Amesema kuwa endapo vigezo hivyo muhimu vinavyoruhusu Chato kuwa mkoa vikikamilika, basi ataitangaza wilaya hiyo kuwa mkoa.
 
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendeleza miradi yote iliyoanza kutekelezwa wilayani Chato, na kuwaomba Wananchi wa wilaya hiyo kuitunza na kuiendeleza miradi hiyo.