Serikali kuja na mpango wa bima ya vifaa tiba saidizi

0
144

Uhitaji wa viungo saidizi ni moja ya changamoto inayohitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kwenye jamii ili kupunguza utegemezi na umasikini kwa watu wenye changamoto hiyo

Hayo yemebainishwa Jijijini Dar es Salaam na rais wa Chama Cha huduma za viungo saidizi na vifaa tiba Leah Mamseri wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau wa afya na watengenezaji wa vifaa tiba saidizi kwa lengo la kubadilishana uzoefu nakujenga uwelewa kwa jamii juu ya vifaa saidizi.

Akimwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika mkutano huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali za Umma na binafsi Luteni Kanali Dkt.Pius Horumpende amesema Serikali kupitia Wizara ya afya itazifanyia kazi changamoto zilizobainishwa katika mkutano huo hasa suala la bima ili kurahisisha huduma kwa watu wenye uhitaji wa vifaa saidizi kwa Ustawi wa taifa.

Kwa Upande wake mhadhiri wa Chuo Cha Wateknolojia Maabarara Viungo Tiba Saidizi kilichopo KCMC Mkoani Kilimanjaro Violet Thadei ameeleza umuhimu wa Serikali na jamii kuhimiza vijana kupata mafunzo juu ya vifaa tiba saidizi ili kupunguza uhaba wa wataalamu kwenye eneo hilo.