Serikali kuendelea na Ukarabati vyuo vya Elimu

0
174

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema miongoni mwa mikakati ya serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha miundombinu ya vyuo vya ualimu inakuwa rafiki na kuwajenga kiuwezo zaidi walimu wanaojifunza.

Profesa Mkenda ameyasema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizindua miuondombinu ya chuo cha ualimu Mpuguso kilichopo Tukuyu mkoani Mbeya.

“Ukarabati na Uboreshaji wa vyuo vya elimu ni sehemu ya mikakati ya serikali yako ya kuboresha elimu ya Tanzania, katika hilo la uboreshaji wa elimu umeshaagiza kwamba elimu yetu izingatie suala la ujuzi ambalo litawaandaa vijana wetu kujiajiri na kuajirika”-amesema Profesa Mkenda.

Aidha Profesa Mkenda ameipongeza serikali ya Canada kwa mchango wake kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania, kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya vyuo vya Ualimu Nchini.

Vyuo vinne kati ya 35 vya ualimu vimekarabatiwa huku ukarabati huo ukiendelea nchi nzima kwa vyuo vyote.