Serikali kuendelea kutoa mikopo vyuo vikuu

0
139

Serikali imeendelea kugharamia utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo iliyopo.

Akijibu Swali la Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo aliyetaka kujua, Serikali ina mkakati gani mahsusi kuhakikisha vijana wote wanaoomba mikopo wanapatiwa, Naibu Waziri wa Elimu Omari Kipanga amesema azma ya Serikali ni kuhakilisha kuwa kila mwanafunzi wa Elimu ya Juu mhitaji anapata mkopo kwa ajili ya kugharamia masomo yake.

Kipanga amesema Katika kutimiza azma hiyo, Serikali imekua ikiongeza fedha za bajeti ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kila mwaka akitolea mfano amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilitoa kiasi cha bilioni 570 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 106 kutoka bilioni 464 ya mwaka 2020/21.