Serikali kuendelea kulinda haki za watoto na wanawake

0
142

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis amesema serikali itaendelea kulinda haki za watoto na kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Naibu Waziri Mwanaidi ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mfano wa kuigwa katika kuwawezesha Wanawake na kwamba kwa sasa kuna wanawake wanaofanya biashara kubwa baada ya kuwezeshwa.

Ameongeza kuwa wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum itaendelea kupita katika mikoa mbalimbali ili kujua mahitaji ya wanawake na kusaidia kuwaunganisha katika kufanya Kazi za ujasiriamali.

Tangu kuanzishwa kwake EOTF imesaidia zaidi ya wanawake elfu sita katika nyanja mbalimbali.