Serikali kuanzisha makumbusho maalum

0
370

Serikali imejipanga kuanzisha makumbusho maalum katika uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kuhifadhi taarifa na picha za Wanamichezo walioliletea Taifa heshima katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza alipokuwa akijibu swali la  Mbunge Ester Mahawe aliyetaka kujua ni lini serikali itaandaa utaratibu wa kuwaenzi wanariadha nchini.

Naibu Waziri Shonza ameliambia Bunge kuwa serikali inawatambua na kuwaenzi wanamichezo wote ambao wameiletea nchi sifa akiwemo Mwanariadha Filbert Bayi aliyevunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 mwaka 1974 na Jumaa Ikanga ambaye ni mshindi wa Medali ya Shaba kwenye Mashindano ya All- Africa Games mwaka 1978 na Medali ya Fedha katika  Michezo ya Olimpiki mwaka 1980 kwa mbio za mita Elfu Tano.