Serikali imefanya mazungumzo na nchi za Vietnam…

0
335

Serikali imefanya mazungumzo na nchi za Vietnam na Misri kwa lengo la kupata wanunuzi wa zao la tumbaku ili kuwawezesha wakulima kupata soko la uhakika wa zao hilo

Hayo yamebainisha na waziri Mkuu Kassim Majaliwa  mjini tabora wakati wa mazungumzo kati yake na wadau wa zao la tumbaku kutoka mikoa mbalimbali yaliyokuwa na lengo la kujadili ununuzi wa zao la tumbaku

Kwa sasa Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na kampuni zinazonunua tumbaku nchini ili ziongeze kiwango cha ununuzi ili kuwawezesha wakulima kuzalisha zaidi.

“Wakulima wanahitaji kuzalisha zaidi lakini wanakwamishwa na kiwango wanachowekewa (ukomo wa uzalishaji) na wanunuzi ambacho ni kidogo ukilinganisha uwezo wa wakulima katika kuzalisha zao hilo.”

Mpaka sasa Serikali inashirikiana na nchi ya Malawi katika utafutaji wa masoko ya zao hilo na tayari kampuni za Malawi zimeahidi kununua tumbaku nchini.