Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, na Uratibu Jenista Mhagama amesema bangi ni tishio nchini kwa kuwa imeendelea kutumiwa zaidi na watu wengi.
Waziri Mhagama ameyasema hayo mkoani Dodoma alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya Dawa za Kulevya nchinii kwa mwaka 2022.
Amesema hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya watu ya kuchanganya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi kwenye vyakula kama biskuiti, keki , asali , majani ya chai na juisi.
Waziri Mhagama amesema kufuatia hali hiyo, Serikali itawasaka wale wote wanaojihusisha na vitendo viuovu vya uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya hali ya Dawa za Kulevya nchini kwa mwaka 2022,
waraibu wa dawa za kulevya 871 wamenufaika na tiba ya dawa za kulevya.