Serengeti kinara tena Afrika

0
323

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ya nchini Tanzania imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora katika Bara la Afrika kwa mwaka 2021.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa hifadhi hiyo ya Serengeti kushinda tuzo hiyo.

Tuzo hiyo imetolewa na taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani ambayo ndiyo muandaaji wa tuzo hiyo kila mwaka.

Kwa mara ya kwanza Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilishinda tuzo hiyo ya kuwa hifadhi bora katika bara la Afrika mwaka 2019 na kwa mara ya pili ilikuwa mwaka 2020.

📸 @fredshirmaphotography

Hifadhi hiyo inapita katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Mara pamoja na Shinyanga na inapakana na nchi ya Kenya.