Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amesema katiba na sheria sio vitu pekee vinavyosaidia kushinda chaguzi mbalimbali, bali pia sera nzuri, usimamizi mzuri wa sera hizo pamoja na mipango sahihi.
Kinana amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa mkutano wake na wanachama wa CCM pamoja na wananchi mbalimbali.
Amesema CCM inazingatia na kusimamia sheria na haki kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu mwaka 2025 ili kuhakikisha amani inadumishwa nchini.
Tupo Mbashara kupitia TBC1, TBC Taifa na mitandao ya kijamii kwa anwani ya TBConline.