Sera Mpya Ya Vijana Zanzibar Mbioni Kuzinduliwa

0
181

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi amesema matayarisho ya sera mpya ya maendeleo ya Vijana Zanzibar yamekamilika na itazinduliwa hivi karibuni na kuanza kazi rasmi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana kimataifa, na kupokea maandamano ya Vijana kutoka taasisi mbalimbali za Vijana katika viwanja vya Maisara, Zanzibar.

Ametoa wito kwa taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Vijana na Mazingira kuendelea kuwekeza katika kuimarisha elimu na uchumi wa kijani kwa Vijana.