Septemba JWTZ itatimiza miaka 60

0
111

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Muungano umewezesha kulinda Uhuru na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, lakini pia kupitia umoja wa Watanzania na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mipaka ya nchi imelindwa na ipo salama.

Akilihutubia Taifa kuelekea sherehe za miaka 60 ya Muungano Rais Samia ameongeza kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ifikapo mwezi Septemba mwaka huu litatimiza miaka 60 tangu kuundwa kwake na kwamba wajibu wa Serikali ni kuendelea kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama ili viendelee kutimiza majukukumu yake ya kulinda mipaka na usalama wa raia na mali zao.

Aidha, Amewahakikishia Watanzania kwamba mipaka ya nchi, uhuru wa Taifa la Tanzania na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar vipo salama ndani ya Muungano.