Sendiga aagiza uhakiki mikopo ya vikundi

0
1406

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Queen Sendiga ameziagiza halmashauri za mkoa huo kufanya uhakiki wa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ambavyo vimepata mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Serikali.

Agizo hilo la Sendiga linafuatia hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya kutorejeshwa zaidi ya shilingi milioni 150 zilizokopwa na vikundi hivyo, hali iliyokwamisha wengine wasikopeshwe.