Sekta ya Sanaa na Madini zaongoza ukuaji 2022

0
116

Wizara ya Fedha na Mipango imesema hadi kufikia Aprili 2023, sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji kwa mwaka 2022 ni pamoja na sanaa na burudani (asilimia 19.0); madini (asilimia 10.9); fedha na bima (asilimia 9.2), malazi na huduma ya chakula (asilimia 9.0), na umeme (asilimia 7.6).

Akiwasilisha Bungeni jijini Dodoma taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2023/2024,
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba
amesema kuwa kutokana na hatua madhubuti zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali thamani ya Pato ghafi la Taifa linatarajiwa kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 85.42 mwaka 2023/2024.