Sekta ya maji yang’ara mbio za mwenge wa uhuru “yafanya vizuri kuliko sekta zote”

0
270

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka huu Sahili Geraruma amemwaga pongezi kwa sekta ya maji.

“Katika sekta ambazo Mwenge wa Uhuru umezifanyia kazi mwaka 2022 sekta iliyofanya vizuri zaidi ni sekta ya maji, maji yanapatika na fedha zilizowekezwa katika sekta hii thamani yake inaonekana,
taratibu za malipo na manunuzi zinafuwatwa, nyaraka za utekelezaji wa miradi ya maji zinahifadhiwa vizuri, watendaji wake wanatimiza wajibu wao na wananchi wanaridhika na huduma ya maji.” amesema Geraruma

https://www.instagram.com/reel/CjsLRIkP8WK/?igshid=YmMyMTA2M2Y%3D

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka huu Sahili Geraruma ameyasema hayo mkoani Kagera wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.