Sasa tunauza nyama Dubai, Saudi Arabia

0
251

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameisaidia wizara hiyo kupandisha bajeti kutoka shilingi bilioni 66.5 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 295.9.

Hatua hiyo amesema imeisaidia wizara hiyo kupiga hatua kwenye utendaji wa kazi na moja ya mafanikio ikiwa ni Tanzania kupeleka nyama nchi za Dubai na Saudia.

Waziri Ulega, amesema hayo Jijini DSM mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye kilele cha Wiki ya Kurasa 365 za Mama Vol. 3 iliyoandaliwa na Clouds Media Group.

Katika hatua nyingine, amesema kuwa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Lindi utakaogharimu shilingi bilioni 289 na kufungua zaidi uchumi wa buluu umefikia asilimia 52

Upande wa mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT), Waziri Ulega amesema mradi huo upande wa mifugo na uvuvi imefanya kazi nzuri kwenye vituo vinane na sasa vinaenda kuwa vituo 13 ambapo vijana walinunuliwa ng’ombe 2,348 na waligawanywa kwenye vituo hivyo vinane ikiwemo Tanga, Mwanza na Kagera na tayari faida ya zaidi ya shilingi milioni 100 imepatikana kwenye mradi huo wa BBT.