Saniniu Laizer: Athibitisha uimara wa Ukuta wa Mererani

0
218

Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kwa kiasi kikubwa kwa kufanya mageuzi makubwa ambayo yemewezesha kulinda na kuwapa watanzania umiliki halali wa rasilimali za Taifa ikiwemo madini ambayo kabla ya miaka mitano ya Serikali ya Rais Magufuli yalikuwa yanamanufaa machache kwa wananchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa mifumo ya karne ya 21 ambayo Rais Magufuli ameiweka katika sekta hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kulinda rasilimali hiyo ambayo ni adhimu kwa taifa na duniani kwa ujumla.

Dkt Abbasi ametolea mfano wa mchimbaji mdogo Saniniu Laizer ambaye Juni 24, 2020 aliishangaza dunia baada ya kuiuzia serikali madini ya Tanzanite yenye uzito wa kilo 15 9 yenye jumla ya thamani ya TZS 7.7 bilioni na lile la Agosti 3, 2020 lenye uzito wa kilo 6.3 ambalo thamani yake ni TZS 4.8 bilioni ni ushuhuda wa mafanikio ya ukuta wa Mirerani ambao Rais Magufuli aliagizwa ujengwe na kuwekewa kamera za ulinzi ili kuepusha utoroshaji wa madini hayo adimu duniani.

Msemaji huyo amesema kupitia madini hayo serikali kupitia Tume ya Madini imekusanya maduhuli ya TZS 881 milioni.

Mfumo mwingine ambao umewezesha kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa makusayo ni kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini ikiwa ni moja ya mafanikio ya Rais Magufuli katika sekta ya madini ambapo hadi Juni, 2020, jumla ya masoko ya madini 31 na vituo vya ununuzi wa madini 39 vilianzishwa maeneo mbalimbali nchini huku faida yake kubwa ikiwa ni kuongezeka kiwango cha madini yanayojulikana kuwa yamezalishwa na kuongezeka kwa mapato ya Serikali.