Sanga aibana serikali hali ya viwanja vya mpira nchini

0
166

Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga (Seneta) ameendelea kupaza sauti juu ya ubovu wa viwanja vya mpira wa miguu nchini.

Akiuliza swali la nyongeza hii leo bungeni jijini Dodoma, Sanga amesema ” Ni mwaka mmoja sasa tangu Rais Samia Suluhu Hassan atoe maelekezo kwa wizara na Chama cha Mapinduzi kuanza kuboresha viwanja nchni hasa eneo la kuchezea, lakini, angu Rais aseme kumekuwa kimya, ni upi mkakati wa serikali kuboresha viwanja hivyo?.

Akikazia swali hilo, Naibu Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu amesema “hata Yanga jana imeshindwa kucheza vizuri pale Mwanza kutokana na uwanja mbovu”.

https://www.youtube.com/watch?v=YIwFGg8t9jk

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul amesema “Serikali inaendelea na majadiliano na Chama Cha Mapinduzi kuanza matengenezo kwa viwanja saba na fedha zimeanza kutengwa kwenye bajeti ya mwaka huu.”