Samia kwenye miaka 20 ya Baraza la Usalama Afrika

0
209

Rais Samia Suluhu Hassan amefika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC-AU).

Rais Samia ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa mwezi Mei na Tanzania ni kati ya nchi 15 tu ambazo ni wajumbe wa Baraza hilo miongoni mwa nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika.