Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga, Omary Mgumba ametoa rai kwa wananchi wa mkoa huo kusaidia kuokoa maisha ya watu pindi inapotokea ajali, badala ya kupora fedha na mali za watu waliofariki dunia ama kujeruhiwa.
Mgumba ametoa kauli hiyo wilayani Korogwe mara baada ya kutembelea eneo la ajali na kuzungumza na baadhi ya ndugu wa marehemu wa ajali iliyotokea wilayani humo ambao wao waliopanda gari nyingine ya nyuma tofauti ya ile iliyopata ajali.
Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 17 wakiwemo 14 wa familia moja waliokuwa wakisafirisha mwili wa marehemu kutoka Dar es Salaam kuelekea Rombo mkoani Kilimanjaro.