Mchezaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane hatoshiriki michuano ya Kombe la FIFA la Dunia linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 20 mwaka huu.
Mane amefanyiwa upasuaji siku ya jana huko Munich na madaktari wamethitisha hawezi kupona kwa wakati na kuichezea timu yake ya Taifa katika fainali hizo za Qatar.
Hapo awali kocha mkuu wa Senegal, Aliou Cisse alimjumuisha katika kikosi cha wachezaji 26 watakaoshiriki katika fainali hizo mwaka huu.
Taarifa ya kukosekana kwa Mane, ambaye ni mchezaji bora wa Afrika mara mbili, katika kikosi hicho cha Simba wa Teranga zimepokelewa kwa mshtuko mkubwa nchini kwao Senegal na Afrika kwa ujumla.