Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake wamefikishwa kwa mara nyingine tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu mashtaka yanayowakali.
Kwa mara ya kwanza Sabaya na wenzake walifikishwa mahakamani hapo tarehe 4 mwezi huu na kusomewa mashtaka matano ambayo ni pamoja na uhujumu uchumi na kuongoza magenge ya uhalifu.