Sabaya apinga vikali ukatili dhidi ya watoto

0
245

Na Sauda Shimbo

Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameyataka mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini kuacha kutetea vitendo vya ukatili kwa watoto.

Badala yake, Sabaya ameyataka mashirika hayo kutoa elimu kwa wananchi juu ya vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto ili kupunguza kasi ya vitendo hivyo katika jamii..

Hayo yamesisitizwa leo Januari 28, wakati Sabaya akizindua kampeni ya ulinzi wa mtoto wilayani humo na kuongeza kuwa hatua hiyo itasaidia watoto kujitambua pamoja na kupunguza vitendo vya ukatili kwao.

https://youtu.be/7lQ13B_irjc

Sabaya amesema kazi ya Mashirika ya haki ya binadamu ni kuhakikisha inazuia vitendo vya ukatili kwa watoto visitokee na sio kusubiri vitokee ndio waaanze kupaza sauti zao katika jamii.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya asema hatosita kumchukulia hatua mganga wa kienyeji atakayebainika kuwalaghai baadhi ya wanaume wilayani humo kushiriki katika vitendo vya kikatili dhidi ya watoto wadogo kwa lengo la kujipatia utajiri.