Akiwasilisha mchango wa hoja ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC), Mbunge wa jimbo la Vunjo Dkt. Charles Kimei amesema ipo sababu ya benki kutengeneza faida ila hazichochei ukuaji wa pato la Taifa.
Dkt. Kimei amesema benki zilizopo nchini zimeshindwa kuchochea ukuaji wa pato la Taifa kwa sababu zimeacha kujikita katika kukopesha sekta za kibiashara ambazo ndio wazalishaji na kujikita zaidi kukopesha sekta binafsi inaotegemea mishahara pekee.
Amesema hata hivyo benki hizo zina kimbizana kuwakopesha waajiriwa wa Serikalini ili kutengeneza faida bila ya kuwa na [risk] kwa kuwa lazima mshahara utaingia kwenye akaunti ya benki kisha ukatwe tofauti na mteja anayefuatiliwa awasishe mwenyewe marejesho ya mkopo.