Sababu tahasusi kuongezeka kutoka 18 hadi 71 zaelezwa

0
718

Kufuatia maboresho ya sera ya elimu na mabadiliko ya mitaala, kutakuwa na ongezeko la tahasusi kutoka 18 za sasa hadi 71 kwa wanafunzi wanaohitimu masomo ya sekondari.

Akitoa mada kwenye kikao cha mazungumzo baina ya maofisa wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na wahariri wa habari leo Machi 7, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Anna Komba amesema tahasusi zimeongezeka kutokana na kuongezeka kwa masomo yakiwemo ya amali.

Mbali na masomo ya amali (ufundi) masomo mengine yanayoongezeka ni kama ya lugha za Kichina, Kiarabu na Kifaransa; masomo ya maadili; Jiografia na mazingira; sanaa na michezo.

Lakini pia somo la ujasiriamali litakuwa la lazima kwa wanafunzi wote wa sekondari.