Ruvu Shooting yaiadhibu Polisi Tanzania 1-0

0
350

Barcelona ya Tanzania, Ruvu Shooting imeondoka na alama tatu katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam baada ya kuifunga Polisi Tanzania 1-0.

Goli pekee na la ushindi kwa wazee wa Mpapaso limefungwa na Abalkassim Suleiman dakika ya 48 ya mchezo.

Kwa ushindi wa leo Ruvu Shooting imefikisha alama 6 baada ya mechi nne zilizotosha kuipandisha hadi nafasi ya 7 ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kwa upande wa Polisi Tanzania ipo nafasi ya 12 ikiwa na alama mbili baada ya kushuka dimbani mara nne.