‘Royal Tour’ kuitangaza Tanzania Kimataifa

Utalii Zanzibar

0
207

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameanza rasmi kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania Kimataifa

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya kuratibu mpango wa kuitangaza Tanzania kimataifa Katibu Mkuu wa Wizara ya habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Rais Samia atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya Utalii, uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo nchini

Zoezi la kurekodi kwa kipindi cha Royal Tour limeanza rasmi tarehe 28 Agosti 2021 kwa kurekodi baadhi ya maeneo yenye vivutio vya utalii na uwekezaji katika visiwa vya Zanzibar