Redio ya jamii TBC Arusha yatimiza miaka 3

0
138

Wasikilizaji wa redio ya
jamii TBC Arusha wameeleza kuridhishwa na usikivu wa redio hiyo pamoja vipindi vinavyotangazwa.

Wakizungumza jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa redio hiyo, baadhi ya wasikilizaji hao wamesema redio hiyo imewasaidia kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali.

Mbali na kutoa pongezi hizo, Wasikilizaji hao wameomba kuboreshwa kwa usikivu wa matangazo katika baadhi ya maeneo.

Mwakilishi wa dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi mkoani Arusha, – Inspekta Shabani Shabani amesema kupitia redio hiyo, jamii imepata elimu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake msimamizi wa redio ya jamii TBC Arusha, – Yesaya Mwambelo amesema redio hiyo imewasaidia wasanii wachanga kupata fursa ya kutangaza kazi zao.

Anna Kwambaza ni Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kaskazini, ambaye amesema kuwa redio hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuwakutanisha pamoja Wananchi ili waweze kupata elimu kwa njia redio.