RC Tanga atembelea Msomera

0
177

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Burian ametembelea kijiji cha Msomera kilichopo katika wilaya ya Handeni kwa lengo na kuzungumza na na kusikiliza kero za wananchi waliohamia katika eneo hilo kwa hiari wakitokea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Katika ziara yake Mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga pia anakagua maendeleo ya miradi mbalimbali katika kijiji hicho cha Msomera.

Dkt. Batilda tayari ametembelea baadhi ya makazi mapya ya wananchi hao wa Msomera waliohamia kutoka Ngorongoro na kusikiliza kero zao na kuahidi kuzifanyia kazi.

Eneo jingine alilotembelea ni Shule ya Msingi Mkababu iliyopo kijijini hapo na kupanda mti ikiwa ni kuunga mkono kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 inayosisitiza utunzaji wa mazingira.