Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewasimamisha kazi watumishi nane wa serikali ili kupisha uchunguzi,baada ya kubaini kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha ulioisababishia hasara serikali.
Kati ya watumishi hao, sita wanatoka ofisi ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika kituo cha pamoja cha forodha cha mpaka wa Horohoro, mmoja anatoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na mwingine anatoka ofisi ya mifugo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa katika mpaka huo.
Kabla ya kufikia uamuzi huo, kamati ya ulinzi na usalama mkoa iliunda tume rasmi iliyoanza kazi ya uchunguzi Septemba 18, mwaka huu, na kubaini kuwepo kwa upotevu wa mapato na uzembe unaofanywa na watumishi hao ambao ni Meneja wa Forodha wa Mkoa wa Tanga Edward Ndupa, Afisa forodha mfawidhi Bakari Athumani, Danda Danda,Julia’s Asila,Bakari Ngoso. Wengine ni Afisa mifugo Nicodemus Kiharus na Michael Katanda TBS.