Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martin Shigela amewaomba Watanzania wa Dini zote kuendelea kuwaombea viongozi wa Kitaifa ili kuendelea kuisimamia Serikali ili kuongoza kwa Amani na kuleta maendeleo kwa watanzania na Taifa kwa ujumla
Shigela ameyasema hayo wakati akitoa Salamu za Serikali kwenye Ibada ya Pasaka inayofanyika Kitaifa katika Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la Mashariki Ushirika wa Morogoro mjini, ambapo amewaomba Watanzania kuendelea kushikamana Katika kujenga Taifa na kutoa ushirikiano kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaendelea kutafuta fursa za kiuchumi nje ya mipaka ya Tanzania
Aidha Shigela amesema, Rais Samai anatarajia kuzindua filamu ya Royal Tour Nchini Marekani ambayo itasaidia kutangaza utalii wa Tanzania na kuvutia wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali kuja kuwekeza Tanzania na kusaidia kukuza uchumi wa watu na Taifa kwa ujumla.
Amewakumbusha Watanzania kusheherekea Sikuu ya Pasaka kwa utilivu bila kufanya vitendo vya uvunjifu wa Amani na kuongeza kuwa kwa Mkoa wa Morogoro kamati ya ulinzi na usalama ipo imara kulinda amani na ya raia na mali zao.