RC Ruvuma : Tuna ziada ya chakula

0
199

Mkuu  wa mkoa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema, mkoa huo una chakula cha kuwatosheleza wananchi wake kwa msimu wa 2022/2023.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Ruvuma, Kanali Thomas amesema, katika msimu wa mwaka 2021/2022 mkoa huo ulizalisha chakula zaidi ya tani  milioni 1.2.

Amesema mahitaji ya chakula mkoani Ruvuma kwa msimu wa mwaka 2022/2023 ni takribani tani Laki 4 na elfu 70 na hivyo kuufanya mkoa huo kuwa na ziada ya chakula zaidi ya tani Laki 7 na elfu 80.

Aidha amesema chakula ambacho kilizalishwa katika msimu wa mwaka 2021/2022 kinatumika katika msimu huu wa mwaka 2022/2023 na kuongeza kuwa mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara.