RC Makalla awapongeza DAWASA kwa utatuzi wa kero za maji pembezoni mwa Dar

0
129

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutatua kero za maji Dar es Salaam.

RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara kwenye Bohari ya Vifaa ya DAWASA ambapo pia amekabidhi hundi ya shilingi milioni 232 kwa wakazi saba wa eneo la Mshikamano waliokubali kuacha maeneo yao kupisha mradi wa ujenzi wa tenki la Maji Mshikamano.

Makalla ameshuhudia shehena ya vifaa vya kufikisha huduma ya maji kwa wananchi na kusema shilingi bilion 5.4 za Mradi wa Maji Mshikamano zinakwenda kumaliza tatizo la maji Jimbo la Kibamba.