RC Makalla awahakikishia Waislamu na Watanzania usalama Mkoa wa Dar

0
308

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makalla, amewataka waislamu kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr bila woga kuhofia vijana wanaofanya uhalifu maarufu kama panya road na kueleza kuwa hali sasa ni shwari na hakuna haja ya wakazi wa Dar es Salaam kuhofia juu ya kundi hilo.

Makalla ameyasema hayo kwenye Baraza la Eid El Fitr kitaifa jijini Dar es Salaam na kusema kuwa ulinzi umeimarika kila mahali ukisimamiwa na kamati ya ulinzi Mkoa huo na kusema kuwa hali ni shwari tangu alipotoa onyo kwa kundi hilo liliibuka na kujeruhi watu na kupora mali zao.

Pia Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuchapa kazi ikiwa ni sehemu ya kazi yake ya kuwatumikia Watanzania bila kuchoka akieleza namna Rais Samia alivyoshiriki Swala ya Eid El Fitr kitaifa jijini Dar es Salaam na kuenda Arusha kushiriki mkutano wa Waandishi wa Habari na kurudi Dar es Salaam kushiriki Baraza la Eid.