RC Kunenge aanza na wakazi wa Pugu, Dar es Salaam

0
319

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Pugu Stesheni ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.

Katika ziara hiyo RC Kunenge amepokea changamoto mbalimbali ikiwemo za elimu, miundombinu, maji, umeme, afya, migogoro mbalimbali na changamoto za kisheria ambapo zipo alizotatua papo kwa papo na nyingine kuzipatia utatuzi kwa kuwaelekea watendaji kuhakikisha wanazishughulikia Mara moja.

Kwenye ziara hiyo RC Kunenge aliambatana na watendaji mbalimbali wa Mkoa akiwemo katibu tawala wa Mkoa, wakuu wa idara pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala.