RC Chalamila: Hatutoingilia bei ya barakoa za kushona

0
467

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kamwe hatoingilia bei za barakoa zinazoshonwa na vitambaa kwa kuwapa bei elekezi kwani ni moja ya fursa za ajira kwa wajasiriamali.

Chalamila ameyasema hayo leo wakati akizungumzia hali ya mapambano ya virusi vya corona, ambapo barakoa moja ya kushonwa mkoani humo inauzwa kati ya shilingi 2,500 hadi 3,000.

Ametoa rai kwa wakulima wa zao la tangawizi kutumia fursa ya uanzishwaji viwanda vya usindikaji zao hilo kutokana kuwa na wateja wengi zaidi katika kipindi hiki cha janga la corona ili waweze pata soko la ndani na nje.

Aidha, amewaonya baadhi ya watu hasa abiria wa bajaji na pikipiki na wanaokwenda kwenye masoko na vituo vya mabasi kuhusu kupuuzia uvaaji wa barakoa.

Chalamila amesisitiza wagonjwa waliopo mkoani Mbeya ni wanne na wote wanaendelea vizuri. Akizungumza na waandishi amewasihi kuendelea kuchukua tahadhari wakati wakiendelea na majukumu.