Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amewataka madiwani wa baraza la Halmashauri ya Chunya kusimamia na kufuatilia wezi wanaotorosha dhahabu nje ya wilaya na mkoa, na kuwataka viongozi wanaosimamia zoezi hilo kuendelea kuwa waminifu katika kazi zao.
Chalamila amezungumza hayo wakati wa uzinduzi wa baraza jipya la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Chunya, uzinduzi ulioenda sanjari na kula kiapo cha utii kwa madiwani hao.
Aidha ametoa rai kwa madiwani hao juu usimamizi wa miradi ya maendeleo likiwepo suala la utoroshaji dhahabu nje ya wilaya.
Viongozi wapya wa baraza hilo akiwemo Mwenyekiti Halmashauri amesema watahakikisha vitendo vyote viovu ndani ya Halmashauri hiyo vinakoma kwani wameapa kuwa waadilifu.