Rasmi Simba yaachana na Haji Manara

0
160

Klabu ya soka ya Simba imeachana na aliyekuwa mkuu wa idara ya habari na mahusiano ya Klabu hiyo Haji Manara na kumtangaza Ezekiel Kamwaga kukaimu nafasi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo leo Julai 28 imeeleza kuwa, Klabu imekubaliana na ombi la Haji(Manara) la kujiuzulu nafasi hiyo ndani ya Klabu.

Mabingwa hao wa nchi kwa mara ya nne mfululizo wamesema Ezekiel (Kamwaga) atashika wadhiwa huo kwa miezi miwili kuanzia leo Julai 28.

Simba wamemshukuru Manara kwa namna alivyojitoa kwa ajili ya Klabu hiyo kongwe hapa nchini na kumtaki heri katika maisha mapya nje ya klabu