Ramani mpya ya Afrika Mashariki

0
240

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesaini mkataba wa kuiruhusu kuwa mwanachama wa saba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na leo wameweza kuongezwa rasmi kwenye ramani ya Afrika Mashariki.

Rais Felix Tshisekedi ametia saini mkataba wa Kongo kujiunga na EAC, Ikulu ya Nairobi nchini Kenya mbele ya Rais Uhuru Kenyatta, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame wa Rwanda.