Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amewasili nchini jioni ya leo Machi 21,2021 tayari kushiriki shughuli ya kitaifa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Marehemu Dkt. John Magufuli.
Rais Mnangagwa amekuwa kiongozi wa nchi wa kwanza kuwasili kwa ajili ya shughuli hiyo kati ya Marais wa nchi kumi ambao wamethibitisha kushiriki hafla ya kitaifa ya kuuaga mwili wa Dkt. Magufuli itakayofanyika kitaifa Mkoani Dodoma.