Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Suleiman Ahmeid Saleh kuwa Katibu wa Rais wa Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Katibu huyo baada ya kumteua Novemba 4, mwaka huu kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo iliyofanyika Ikulu, Zanzibar, akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Hassan Khatib, Naibu Kadhi Mkuu, Sheikh Hassan Othman Ngwali, Viongozi wa Vikosi vya SMZ pamoja na viongozi mbalimbali kutoka idara na taasisi za Serikali.
Kabla ya uteuzi huo katibu huyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.