Rais wa indonesia kuwasili nchini jioni hii

0
161

Rais Joko Widodo wa Indonesia anatarajiwa kuwasili nchini jioni hii kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha maeneo mapya ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ikiwa ni.pamoja na biashara, nishati, afya, kilimo, madini, elimu na uhamiaji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Stergomena Tax amewaambia Waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa, akiwa nchini Rais Widodo pamoja na mambo.mengine atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia.Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam.

Pia atashuhudia kusainiwa kwa hati kadhaa za makubaliano zinazolenga kuimarisha Diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania na Indonesia.