Rais wa Congo awasili DSM

0
207

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi Tshilombo amewasili jijini Dar es Salaam akitokea Zanzibar na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Baada ya kuwasili Rais Felix Tshisekedi ameelekea Ikulu ya Dar es Salaam ambapo huko atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

congo #raiswacongo