RAIS TSHESEKEDI AISHUKURU TANZANIA NA SADC KUFANIKISHA AMANI YA DRC

0
303

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshesekedi amezishukuru nchi wanachama wa SADC ikiwemo Tanzania kwa mchango wao wakati wa kubadilishana madaraka kwa amani zaidi na kwa sasa hali ya amani Kongo inazidi kuimarika licha ya eneo la Mashariki mwa nchi hiyo bado kunatishiwa na kundi la kigaidi.

Aidha Rais Tshesekedi ameziomba nchi wanachama kuimarisha umoja na mshikamano na kushauri kuwa mwisho wa mkutano huo watoke na tamko la kuwa na kundi la kikanda la kukomesha uovu ili kuzidi kuimarisha nchi wanachama kiusalama na uchumi.

Kuhusiana na kauli mbiu ya mkutano huo wa 39 inayosema “Mazingira wezeshi kwa maendeleo endelevu na Jumuishi ya Viwanda, kuongeza Biashara na Ajira Kikanda” Tshesekedi amesema kuwa jumuiya ya Kongo ina mipaka na nchi nyingi na fursa nyingi hupatikana kupitia mabwawa ya nishati na amehahidi ushirikiano na na kushauri kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara ili wananchi waweze kufanya biashara na kujenga uchumi wa jumuiya kwa ujumla.

Pia ameshauri nchi wanachama kuzingatia kilimo pamoja na ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme ili kuweza kufikia azma ya kufanya mapinduzi ya viwanda na anaamini mkutano huo utafikia malengo makubwa ndani ya jumuiya hiyo.

Tshesekedi amepongeza mwenyekiti anayemaliza muda wake na kueleza kuwa Hana mashaka na mwenyekiti mpya Rais Magufuli na agenda yake wa kujenga Viwanda katika ukanda huo wa SADC wanaamini itafikiwa vyema na kumalizia kwa kusema kuwa lazima jumuiya ijipongeze kwa kukichagua Kiswahili kuwa lugha rasmi ya jumuiya hiyo.