Rais Samia : Zingatieni mipango ya nchi

0
225

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi ambao amekua akiwateua kufanya kazi kwa kuzingatia mipango ya nchi.

Rais Samia ametoa kauli hiyo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbal wakiwemo Mawaziri watatu kufuatia mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri aliyoyafanya hivi karibuni pamoja na Wajumbe wa Baraza la Maadili.

Amesema asingependa kuona Viongozi anaowateua wanafanya kazi kwa kufuata nafsi zao badala ya kuzingatia mipango ya nchi.

Amewataka kufanya kazi kwa bidii wakitambua kuwa kazi kubwa iliyopo mbele ni kuhakikksha Taifa linapata maendeleo.

Rais Samia Suluhu Hassan amerejea kauli yake ya kuwataka Viongozi anaowateua kushirikiana na kuepuka migogoro baina yao ama na Wanaowaongoza katika vituo vyao vya kazi.

Mawaziri walioapishwa ni
George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, Damas Ndumbaro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na
Pindi Chana kuwa Waziri Maliasili na Utalii.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.